Testo Nimwage Radhi Feat Harmonize - Mrisho Mpoto feat. Harmonize

Testo della canzone Nimwage Radhi Feat Harmonize (Mrisho Mpoto feat. Harmonize), tratta dall'album Nimwage Radhi Feat Harmonize

(Ayo Lizer)
Furaha isiyo kifani kupata mwandani
Hakika wamependeza
Goma lipo uwanjani, kaibiwa nani
Sa unaachaje kucheza
Ama kweli harusi imefana tena ya kihistoria
Pande zote, baba na mama naona wanashangilia
Ila sitaki kuwa mnafiki jumba bovu kuniangukia
Nina langu la moyoni ningependa kuwaambia
Bi' harusi mashoga wa kukupia hao ni wa kuwaangalia
Wako wale wa hali gani wanakuja kuchungulia
Uwaombe samahani, uwakomeshe wambea
Eti wifi umepika nini na mimi utanigawia
Waambie umepika dagaa zenye pili-pili nyingi
Zinakutosha wewe na mme wako, wao watakimbia
Eh! Aii, shemeji tubu huyo mumeo, usiskize ya fulani
Na hii, ndo meseji sema na mumeo usifuate ya jirani
Kwa furaha niliyonayo
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi (aiyoyo)
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi
Ng'ombe anapoita ndama tunasema kuwa analia
Kupigwa na kulalama havijawahi kusikia
Hakika mmependeza
Mi navyomfahamu bi harusi sipati kusimulia
Nimetokea Ruvuma, Mtoboro, Namtumbo, Lindi, Mtwara mpaka Chatoholi
Nimezisikia sifa za binti huyu Mola amemjalia
Binti hapendi majungu hakika ni nachowaambia
Ukimuazima viatu na gauni anakuachia
Bwana harusi tunakupa mke ukaishi naye vyema nyumbani
Una kitu usimfiche, mwambie tahadhari
Ikiwezekana mkakope mkono uende kinywani
Usimpige mateke kisingizio kitu fulani
Oh, umefanya nini jana hakuliki leo ndani
Mtoto bado mteke usimkomaze kwa ngumi
Ukimshindwa mrudishe, kwao hajaua huyu
Mumeo akienda kazini akirudi salimia
Wala usikae chini chakula kumsukumia
Mkaribishe ndani, hali ukimjulia
Muulize za kazini kwa tabasamu murua
Kisha msindikize bafuni hata kama anapajua
Halafu wewe tafuta kiti jikoni kimbilia
Chukua simu yako meseji ukimtumia
Mwambie asilani bila wewe chakula hakitaingia
Eh! Aii, shemeji tubu huyo mumeo, usiskize ya fulani
Na hii, ndo meseji sema na mumeo usifuate ya jirani
Kwa furaha niliyonayo
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi
Nawaomba niishie hapa, tarishi huwa hafungwi
Naomba nichape lapa, yaliyobaki ni ya makungwi
Niliowakera samahani, kusema ni jukumu langu
Nawaomba muishi kwa amani, hiyo ndio furaha yangu
Mmh, ndoa ni kama safari tuombeane dua
Atuepushe na shari za chini ya jua
Ah, somo yake mwali (ainuke)
Mama yake mwali (ainuke)
Baba yake mwali (ainuke aje kati tulicheze ngoma)
Kaka yake mwali (ainuke)
Dada yake mwali (ainuke)
Shangazi yake mwali (ainuke aje kati tulicheze ngoma)
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi
Niacheni nimwage radhi
Mi nataka nimwage radhi
(Wasafi Records)



Credits
Writer(s):
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link

Disclaimer: i testi sono forniti da Musixmatch.
Per richieste di variazioni o rimozioni è possibile contattare direttamente Musixmatch nel caso tu sia un artista o un publisher.

Elenco artisti

© 2026 Riproduzione riservata. Rockol.com S.r.l.
Policy uso immagini

Rockol

  • Utilizza solo immagini e fotografie rese disponibili a fini promozionali (“for press use”) da case discografiche, agenti di artisti e uffici stampa.
  • Usa le immagini per finalità di critica ed esercizio del diritto di cronaca, in modalità degradata conforme alle prescrizioni della legge sul diritto d'autore, utilizzate ad esclusivo corredo dei propri contenuti informativi.
  • Accetta solo fotografie non esclusive, destinate a utilizzo su testate e, in generale, quelle libere da diritti.
  • Pubblica immagini fotografiche dal vivo concesse in utilizzo da fotografi dei quali viene riportato il copyright.
  • È disponibile a corrispondere all'avente diritto un equo compenso in caso di pubblicazione di fotografie il cui autore sia, all'atto della pubblicazione, ignoto.

Segnalazioni

Vogliate segnalarci immediatamente la eventuali presenza di immagini non rientranti nelle fattispecie di cui sopra, per una nostra rapida valutazione e, ove confermato l’improprio utilizzo, per una immediata rimozione.